Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (alietangulia) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakitembelea mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha,Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.


Serikali imesema mradi wa ujenzi wa jengo la abiria la tatu  umekamilika kwa asilimia 66 na kwamba mradi huo utakamilika Septemba, mwakani kama ilivyopangwa kwa kuwa kwa saasa hakuna kikwazo chochote.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Elias Kwandikwa wakati alipotembelea mradi huo leo, jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa serkali imeshamlipa mkandarasi fedha anazodai na kwa sasa hawana deni.


"Awamu hii ya pili tunajenga uwanja huu kwa fedha zetu za ndani, hii ni ishara tunaelekea kuzuri kwamana itafika mahali tutakuwa na miradii kama hii kwa fedha zetu wenyewe," amesema Kwandikwa.
Msimamizi wa Mradi huo  Mhandisi,Barton Komba(kulia) akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa wakiwa kwenye eneo la mradi huo leo jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...